Searching...
Jumatatu, 9 Desemba 2013

KINYANG'ANYIRO CHA TUSKER PROJECT FAME 6,HOPE WA BURUNDI NDIYE MFALME,MTANZANIA ASHIKA NAFASI YA NNE.

Jana ilikuwa ni Wakati Mgumu sana kuweza kutabili nani ataibuka Kinara wa TPF Season 6 “Take The Stage”, baada ya washiriki Wote walioingia Fainali kuwa Hatari katika kuonesha vipaji Vyao.
Lakini Kubali ukatae, ilikuwa ni lazima apatikane mtu ambaye angeondokoa na Mkwanja mrefu ambao ulikuwa Umeandaliwa kwa ajili ya Mshindi.
Kama ambavyo wengi walitabiri, Mshiriki pekee aliyekuwa akiiwakilisha Nchi ya Burundi, HOPE, ndiye aliibuka Kinara Wa Shindano hilo lililodumu kwa Muda wa Wiki 8, huku akiwapiga Chini Fainalists Wenzake ambao pia walikuwa ni wachungu balaa huku wakiamini kuchukua Fedha hizo nyingi.
AMOS na JOSH kutoka Kenya ndiyo walishika nafasi ya Pili, DEISY EJANG Kutoka Uganda, alidaka nafasi ya Tatu, 
HISIA WA TANZANIA.
 HISIA kutoka Home sweet home Tanzania, akikamata nafasi ya NNe
Ushindi ulianza kutabirika kwa Hope ikiwa ni Ndani ya Wiki ya Nne tu, baada ya kujizolea mashabiki kupitia Vocal lake la kipekee, lilimfanya awe kipenzi cha watu.
TUSKER PROJECT FAME SEASON 6 “TAKE THE STAGE” imemalizika ikiwa Chini ya Principal ERICK WAINANA, ambaye aliifanya kuwa tofauti, na kuwa na Ushindani ambao haujawahi kutokea tangia Ianze.
Mchakato huo Ulianza na washiriki 15, walioanza kusukamana kuanzia OCTOBA 18.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!