
Shughuli ya mazishi ya marehemu Tabu Ley Rochereau gwiji wa Rumba Afrika, inaendelea mjini Kinshasa, DRC.
Viongozi wa serikali ya DRC wamehudhuria mazishi
hayo huku wawakilishi kutoka nchi jirani ya Congo Brazaville pia
wamehudhuria mazishi hayo.
Tabu Ley alifariki mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 76 akipokea matibabu nchini Ubelgiji.
Wengi walimkumbuka Tabu Ley kwa mziki wake na
kwa talanta yake kwa utunzi wa nyimbo zake zilizowagusa watu wengi
Afrika. Tabu Ley amefanyiwa mazishi ya kitaifa
Mwanamziki huyo ambaye pia alikuwa mwanasiasa,
hakuwahi kupona tangu alipougua kiharusi mwaka 2008 na hali yake
iliendelea kuwa mbaya hadi alipofariki Novemba 30.
Alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji kimoja kidogo
Magharibi mwa mkoa wa Bandundu, na hapo ndipo nyota yake ilianza
kung'aa a katika fani ya muziki wa Rumba mapema miaka ya sitini.
Tabu Lei alitaka sana kuwa waziri wa utamaduni
katika serikali ya Laurent-Desire Kabila --babake rais Joseph Kabila,
lakini badala yake akawa naibu gavana wa mji wa Kinshasa.
Alikimbilia usalama wake wakati wa utawala wa
aliyekuwa rais Mobutu Sese Seko kati ya mwaka 1965 to 1997, na mnamo
mwaka 1990, serikali ya Mobutu ikapiga marufu album yake Trop, c'est
trop.
0 comments:
Chapisha Maoni