Searching...
Jumatano, 11 Desemba 2013

BUNDI AENDELEA KULIA MANCHESTER UNITED,ROONEY AGOMA KUFUNGUA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA.

 
 WAYNE ROONEY.
Mchezaji wa kimataifa wa England amegoma kufungulia mazungumzo ya kuongeza mkataba wa kukipiga na klabu yake ya sasa ya manchester united ambapo mkataba wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao ambapo klabu hiyo inataka kumpa mkataba wa miaka minne.
DAVID MOYES - KOCHA WA MANCHESTER UNITED
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mwezi uliopita ilikua Rooney apewe mkataba wa miaka minne ambapo ilikua aendelee kujiingizia kiasi cha paundi laki mbili na nusu kwa wikilakini magazeti yaliandika kwamba habari za uhakika Rooney amegoma kabisa hata kukutana na wawakilishi wa Manchester United.
 
JOSE MOURINHO-KOCHA WA CHELSEA
 Hata hivyo klabu ya Chelsea inasemekana ndilo chaguo namba moja la Rooney na taarifa za uhakika zinasema tayari Mourinho amemtengea donge nono sana la uhamisho ili kumuwezesha kutua Chelsea kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
ARSENE WENGER - KOCHA WA ARSENAL.
ukiachilia mbali Chelsea kumtaka Rooney lakini pia klabu za Arsenal na Real Madrid nao wameonyesha kila dalili za kuitaka saini ya mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri Old Trfaffor.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!