Msafara wa gari lililobeba Jeneza lililochukua mwili wa Nelson Mandela lilipitishwa katika mitaa ya
mjini Pretoria nchini Afrika kusini hadi katika jengo la Umoja, jengo
ambalo ni makao makuu ya serikali.
Kwa muda wa siku tatu wananchi wa Afrika kusini watapata fursa ya kuuona
mwili wa kiongozi wao huyo aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya
kuwakomboa Waafrika kusini.
Viongozi kutoka mataifa ya kigeni walioko hivi sasa nchini Afrika kusini
kwa ajili ya tukio la kumbukumbu ya Nelson Mandela pamoja na wana
familia wamekuwa wa kwanza kuweza kuuona mwili wa Mandela katika jeneza.
Umma umeanza kuruhusiwa kuingia katika jengo hilo kuanzia mchana wa
leo(11.12.2013).
Jeneza litafunguliwa na uso wa Mandela utaonekana , licha ya kuwa ni kupitia kioo ambacho kitauhifadhi mwili wake.
Kabla ya gari lililochukua mwili wa Mandela kuwasili, eneo lenye safu ya
viti vilivyopangwa nusu duara mbele ya jengo hilo la serikali , eneo la
uwanja ambalo limepewa jina la Nelson Mandela , lilikuwa na kelele za
helikopta zilizokuwa zikizunguka angani.
ULINZI UKIWA UMEIMARISHWA KIJIJINI KWA MZEE MADIBA TAYARI KUWAPOKEA VIONGOZI MBALIMBALI WA KIMATAIFA.
Hali ya ukimywa ilitawala katika eneo hilo mara baada ya jeneza
lililouchukua mwili wa Mandela lilipowasili na jeneza hilo lilichukuliwa
hadi katika eneo maalum lililoinuliwa kiasi ya mita saba na wanajeshi
nane waliovalia nguo za rangi ya zambarau wakiongozwa na kasisi wa jeshi
wakiwakilisha vikosi mbali mbali vya majeshi na polisi.
Bendi ya jeshi ilikuwa ikipiga wimbo wa taifa , wakati polisi kadha
pamoja na wanajeshi wakiwa wamesimama wakitoa heshima zao wakati jeneza
lililokuwa limefunikwa bendera ya Afrika kusini likiingizwa katika jengo
hilo ambalo ni makao makuu ya serikali.
Mandla Mandela.
Mjukuu wa Mandela , Mandla Mandela , aliongoza kundi dogo la
waombolezaji waliovalia nguo nyeusi ambao walitembea kuzunguka jeneza.
Ndugu wengine katika familia ya Mandela pia walihudhuria.
"Ni kitu cha kushangaza kufikiria kuwa miaka 19 iliyopita alitawazwa
kuwa rais katika jengo hilo, na sasa amelala hapa," amesema Paul
Letageng mmoja wa wafanyakazi katika ofisi za serikali kwa hisia kali.
Wakati wa tukio la kumbukumbu ya Mandela hapo jana viongozi kadha
walitoa maelezo yenye hisia kali kuhusiana na yale Mandela
aliyoyasimamia na kuyatenda katika uhai wake.
Katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon amesema Mandela alikuwa mwalimu wetu mkuu.
"Nelson Mandela alikuwa zaidi ya kiongozi shujaa katika wakati wetu huu. Alikuwa mwalimu mkuu. Ametufundisha kwa mifano."
Mamia ya Waafrika kusini walijipanga katika sehemu ya njia iliyotumika
kuchukua mwili wa Mandela kutoka katika eneo la kuhifadhia maiti
hospitalini hadi katika jengo hilo la serikali.
Mwili wa Mandela utakuwa unapelekwa katika hospitali ya jeshi hadi
katika jengo hilo ambalo ni makao makuu ya serikali , hatua
itakayochukua kiasi ya saa moja kila siku. Siku ya Alhamis na Ijumaa
wananchi wataruhusiwa kutoa heshima zao kuanzia saa mbili asubuhi saa za
Afrika kusini hadi saa tisa na nusu jioni.
mazishi ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumapili katika kijiji cha asili anakotoka Mandela cha Qunu ambapo watu wapatao 15,000
CREDIT-DW SWAHILI.
0 comments:
Chapisha Maoni