Toyota Cresta lenye namba za usajili T888 BWW mali ya Vailet Mathias lililotolewa upepo na kusababisha ugomvi baina ya polisi na mmiliki huyo aliyepigwa risasi begani. |
NYUMA ya sakata la mwanamke, Violet Mathias, mkazi wa PPF jijini hapa
aliyepigwa risasi begani na polisi baada ya kukaidi amri ya kutopaki
gari sehemu isiyoruhusiwa katika Benki ya CRDB Jengo la TRA hivi
karibuni, limeibua mambo mapya nyuma ya pazia.
Ilidaiwa kuwa, polisi alimuwahi mwanamke huyo baada ya yeye kuchukua bastola kwenye gari na kuikoki tayari kumfyatulia, akapigwa yeye mkononi.
Habari nyuma ya pazia zilidai kuwa, siku hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke huyo na watu wengine kuzuiwa kupaki sehemu hiyo ambayo ina mlango wa kuingilia mkono wa kushoto wa Jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo ndani yake kuna Benki ya CRDB.
Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, Violet alipaki tena gari eneo hilo na alipofuatwa na kuambiwa akalisogeze alikataa kwa nyodo.
Ilidaiwa kuwa baada ya kunusurika kifo Violet au Vai kama anavyojulikana jijini hapa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambayo ipo hatua kadhaa kutoka eneo la tukio.
Habari zilidai kuwa katika kuficha tukio hilo, Violet ambaye ni mwanamke mrembo na mfanyabiashara wa madini na kusafirisha watalii alihamishwa ‘kiaina’ katika hospitali hiyo na kupelekwa Hospitali ya Seliani iliyopo jijini hapo.
Hata hivyo, katika tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kumekuwa na usiri mkubwa wa waandishi wa habari kujua wodi aliyolazwa kwa kuwa ndugu hawataki apigwe picha.
Kutokana na kuzagaa kwa silaha mkoani hapa, jeshi la polisi limeombwa kukusanya silaha zisizo milikiwa kihalali kutoka mikononi mwa raia ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.
0 comments:
Chapisha Maoni