Searching...
Alhamisi, 5 Septemba 2013

WEMA SEPETU, KAJALA, DULLY SYKES NA MASUPERSTAR WENGINE WALA BATA NA SKY LIGHT BAND KWENYE KIOTA CHA THAI VILLAGE.

IMG_4335
Vijana wa Skylight Band kutoka kushoto ni Rappa Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakishambulia jukwaa Ijumaa iliyopita kwenye uwanja wao wa nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar. Pia usikose Family Day Bonanza la Skylight Band Escape 2 kila siku za Jumapili kuanzia saa kumi jioni.
IMG_4346
Watuache kwa raha zetu mziki umekolea.....Mdau Emma na The Big Boss wakisakata rhumba.
IMG_4347
Rappa Joniko Flower akiwakimbiza mashabiki wa Skylight Band na Style ya Mukanda wa chuma chuma.....!
IMG_4352
Shabiki wa Skylight Band akionyesha manjonjo yake jukwaani.....Palinoga ni balaaa.
IMG_4354
Hapo sasa twende kazi...marafiki wakimshangilia rafiki yao jukwaani.
IMG_4404
Diva Aneth Kushaba AK47 akikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band.
IMG_4374
Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lucos akitoa burudani huku akisindikizwa na mwimbaji mwenzake Digna.
IMG_4421
Superstar Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa na mrembo wa kizungu pamoja na JEMBE wakishow love mbele ya camera yetu.
IMG_4412
Maimatha wa Jesse akishow love na marafiki alipotinga kwenye kiota cha Thai Village kuanza week end yake na burudani za Skylight Band.
IMG_4425
William Malecela a.k.a LEMUTUZ akishow love na mdau Alois Ngonyani na marafiki ndani ya kiota cha Thai Village.
IMG_4370
Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
IMG_4427
Burudani ikiendele Sam Mapenzi a.k.a sukari ya warembo akifanya yake jukwaani.
IMG_4433
Sam Mapenzi akicheza sambamba na mashabiki wa Skylight Band..... palikuwa hapatoshi.
IMG_4447
Utamu ulipokolea wengine walipiga nduru, wengine walishika vichwa.......Hapana chezea Skylight Band.
IMG_4452
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo alishika atamu kuwarusha mashabiki wa Skylight Band.
IMG_4456
Wema Sepetu akiwasili kiota cha Thai Village na kuwasabahi vijana wa Skylight Band kuonyesha kuwakubali kwa burudani yao.
IMG_4460
Furaha na tabasamu bashasha vilitawala usoni kwa mwanadada Wema Sepetu.
IMG_4466
Wema Sepetu hakuja peke yake aliambatana na swahiba wake mkubwa Kajala.
IMG_4471
IMG_4484
Kila mtu alijinafasi kwa style ya aina yake.....wenye kupinda mgongo haya kwa raha zao.
IMG_4494
Wema Sepetu akifurahi jambo na mashabiki wake ndani ya kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar.
IMG_4498
Mduara ulihusika kama kawaida.
IMG_4504 wadau wakiserebuka na skylight band
IMG_4507
Wema Sepetu na Kajala wakibadilishana mawazo huku burudani ya Skylight Band ikiendelea.
IMG_4546
Pichani juu na chini ni Wema Sepetu akimpagawisha Sam Mapenzi wa Skylight Band
IMG_4552
Sam Mapenzi akimwimbia Wema Sepetu ndani kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar Juma lililopita.
IMG_4555
Petit Man naye hakukubali kulishindwa akamuonyesha Wema ufundi wake kwa kusakata Sebene la Skylight Band.
IMG_4473
Ukumbi ulilipuka ni nomaaa kama inavyoonekana pichani.
IMG_4477
Wadau wa Skylight Band bila kukosa wakiwakilisha Kijitonyama.
IMG_4478
Wadau wa ukweli wenye mapenzi na Skylight Band camera yetu iliwamulika.
IMG_4482
Wasanii wa Bongo Flava kutoka kushoto ni Shetta, TID pamoja na Dully Sykes nao walikuja kula bata na Band ya vijana, wakubwa kwa watoto yenywe Swaggaz za ukweeeh Skylight Band.
IMG_4539
Wema Sepetu na William Malecela a.k.a LEMUTUZ wakishow love.
IMG_4535
Benny Kinyaiya, William Malecela na Wema Sepetu.
IMG_4542
Divas wa Skylight Band kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Digna pamoja na Mary Lucos wakishow love.
IMG_4454
Mdau Cathbert Kajuna wa Kajuna Blog naye alikuwepo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!