Searching...
Jumamosi, 14 Septemba 2013

UNYAMAAA!!!! MAMA MKUBWA AMUUNGUZA VIDOLE MTOTO KISHA KADOKOA MBOGA

Mtoto Winfrida Nicolaus aliyeunguzwa na mke wa baba yake mkubwa ambaye ni askari polisi, kwa madai ya kudokoa mboga akiwa amebebwa na Bloger Sengo
“ Alinishika na kusema eti nimedokoa nyama minofu miwili niliposema sio mimi alinichapa fimbo kila sehemu na akanifunga kitamba na kunimwagia mafuta ya taa na kunichoma na moto wa kiberiti nililia lakini alikuwa nananifungia ndani ili watu wasinione” alisimulia mtoto huyo

Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha Foundation Karibu Tanzania Johanes Emmanuel (kulia) akizungumzia sakata hilo.
Naye Afisa Ustawi wa Jamiii Kituo cha Foundation Karibu Tanzania Johanes Emmanuel alisema kuwa kutokana na kuzidi kwa kasi ya ukatili Jijini Mwanza kutajwa kuongezeka kumepelekea Kituo hicho kupokea watoto waliofanyiwa ukatili majumbani ambapo imevuka malengo kwa asilimia 25 ya mwaka ya kutegemea kuokoa watoto 40 na sasa wanaokoa watoto na kupokea wapatao 100 kwa mwaka.
Picha za watoto waliokumbana na ukatili.
Afisa Emmanuel amesema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2011 kimeokoa zaidi ya watoto 120 waliounguzwa kwa moto na mpaka sasa watoto 94 wamerudi makwao na 27 ndiyo walio bakia kituoni hapo wakiendelea na matibabu na kusubilia kupewa elimu wazazi na walezi wao waliowafanya ukatili jambo ambalo huwaogopesha watoto hao wakati wakiambiwa kuchukuliwa kurudi majumbani mwao.
Inasikitisha kwa mtoto huyu aliyekumbana na ukatili wa kucharangwa mikono kama ukataji muwa unavyokuwa.
“Ukatiili huu upo kwenye majumba na kitendo cha watoto kufichwa majumbani baada ya kutendewa ukatili na kupatwa na majeraha husababisha wengi wao kupata ulemavu wa kudumu kutokana na kutelekezwa kwa kukosa Tiba ya haraka naya uhakika kwa majeraha waliyopata hali ambayo huwachukua muda mrefu kupona hasa wanapochukuliwa na Kituo hiki kuanza kufanyiwa utaratibu wa matibabu” alieleza.

 
Back to top!