TANGA, Tanzania
KAMANDA wa Polisi mstaafu wa Mkoa wa Tanga, Feith Amour (61)
amefariki dunia mjini hapa baada ya kuugua maradhi ya shinikizo la
damu.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema leo kuwa Amour alifariki dunia jana saa 6.30 usiku katika hospitali ya Safi Medical iliyopo Jijini hapa.
Faith Amour amewahi kuwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga kwa kipindi cha miaka sita hadi kufikia mwa 2006 na baada ya kustaafu alikuwa akiishi Tanga
Feith Amour alizaliwa oktoba 23 mwaka 1952 mtaa wa Kikwajuni Zanzibar na kusoma shule ya msingi St.Monica mwaka 1958 hadi 64 aakajiunga na Sekondari ya Tumekuja Zanzibar na baadaye akasomea ukatibu muhtasi katika chuo cha Magogoni Dar es salaam.
Utumishi katika jeshi la Polisi alianza rasmi mwaka 1970 akiwa Zanzibar na mwaka 1974 akaapata cheo cha mkaguzi msaidizi hatimaye akahamishiwa ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Dar es salaam na mwaka 1983 alihamishiwa Tanga na kuwa mnadhimu namba moja.
Mwaka 1990 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga nafasi aliyotumikia hadi mwaka 2006 alipohamishiwa ofisi ya IGP na alistaafu mwaka 2008 akiwa Kamishna msaidizi wa Polisi ACP.
Mwili wa Feith Amour ambaye ameacha watoto watano na wajukuu wawili ulitarajiwa kusafirishwa leo jumamosi saa 9.00 jioni kupelekwa Kikwajuni Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

0 comments:
Chapisha Maoni