Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza
Gary Hutchinson(kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam juu ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya
Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza
na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Michezo Leonard Tadeo (kushoto).
Mkurugenzi wa Biashara
wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi
jezi ya timu yake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard
Tadeo (kushoto) leo jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo ya awali ya
kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii
na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii
wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki.
0 comments:
Chapisha Maoni