Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu wa EAGT marehemu Moses Kulola katika mazishi yaliyofanyika leo kwenye eneo la uwanja wa Kanisa la EAGT Bugando Mwanza.. |
Rais
Kikwete amemtaja Marehemu Kulola kama mmoja kati ya viongozi
wanaharakati tangu na kabla ya Uhuru waliojitolea maisha yao
kuwaunganisha watanzania kupitia imani yake, akihubi nguzo kuu ya imani
yaani Upendo.
Viongozi
waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri mkuu mstaafu Edward
Lowassa, Katibu mkuu wa CHADEMA Wilbroad Slaa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Evarist Ndikilo, Mwenyekiti wa Chama Cha ADC Lucas Limbu, Wabunge
mbalimbali wa vyama vya siasa, Viongozi mbalimbali wa dini wa Makanisa
ya nchi za Africa Mashariki, Viongozi wa Jeshi pamoja na Wakuu wa Wilaya
mbalimbali Kanda ya Ziwa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Wilbroad Slaa (wa pili toka kushoto mbele) akiwa na mkewe, huku Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (kushoto) akionekana . |
Mwigizaji wa Ze Komedi ambaye pia ni mwimbaji wa njimbo za Injili Emanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiwa na vijana wa kundi lake alitumika kutoa neno kwa njia ya uimbaji. |
Mwimbaji maarufu wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki Flora Mbasha aliimba wimbo mahsusi pamoja na wajukuu wenzake wa Askofu Moses Kulola. |
Viongozi. |
Wanahabari. |
Makamu Askofu Mkuu wa EAGT Asumwise Kayoya Mwaisubila akimwaga udongo kaburini wakati akiongoza ibada ya mazishi ya Askofu Moses Kulola. |
Mke wa Rais wa Tanzania, Mama Salma Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa Kanisa la EAGT marehemu Moses Kulola. |
Katibu mkuu wa CHADEMA Wilbroad Slaa akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa Kanisa la EAGT marehemu Moses Kulola. |
Sala maalum kwaajili ya mazishi. |
Njia kuelekea eneo la tukio viwanja vya EAGT Ushirika wa Bugando Mwanza Tanzania. |
Gari la kwanza kutoka eneo hili lilikuwa la Mhe. Rais JK. ambapo watu wengi walifurika nje ya lango kuu ambalo lilifungwa kutokana na watu walioingia eneo la uwanja kufikia idadi ya usalama. |
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa akitoka eneo la uwanja wa EAGT Ushirika wa Bugando jijini mwanza huku wananchi wakisalimiana naye. |
0 comments:
Chapisha Maoni