PICHA NA MAKTABA
Katika hali ya kushangaza muda huu bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania likiwa linaongozwa na Naibu spika wa bunge hilo mheshimiwa Job Ndugai limesimama kwa zaidi ya dakika 30 huku hali ya fujo ikitawala na mapolisi wa bunge zaidi ya 40 wakiwa wameitwa ndani kumtoa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mheshimiwa Freeman Mbowe.
SINEMA YENYEWE IPO HIVII:-
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na vikao vyake ambapo leo ni mkutano wa 12 kikao cha 08 ambapo kuanzia jana wamekuwa wakijadili muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba 2013 ambao huo ukipita unakua sheria ambayo ndiyo itakayoendesha zoezi zima la kupata katiba mpya,ambapo jana wabunge wa upinzani walitoa hoja ya kuharisha muswada huo kwa madai kwamba wananchi hawajapewa nafasi ya kuchangia.
Leo asubuhi bungeni wabunge wengi waliomba muongozo wa spika ambapo mbunge mmoja alimtaka naibu spika aarishe muswada huo na naibu spika akasema yeye hana mamlaka ya kuahirisha ila bunge lenyewe ndio lenye mamlaka hayo,ambapo aliwahoji ...wanaosema SIYO waseme SIYO.....SIYOOOOOOOO....wanaosema NDIYO waseme NDIYOOOOOOOOO waliosema siyo wameshinda..(alisema naibu spika)
Lakini Mheshimiwa Mnyika akaomba zipigwe kura,naibu spika akakubali zikapigwa kura kwa kuwaita majina wabunge zaidi ya 150 ambapo waliokataa kuuondoa muswada huo wakashinda tena.
MBOWE ASIMAMA.
Mheshimiwa Mbowe asimama na akakataa kukaa,wabunge wote wa upinzani wakasimama kasoro Mrema.
MAASKARI KAENI TAYARI.
Naibu spika aagiza askari wa bunge wajiandae kumtoa nje mheshimiwa Mbowe,wakaingia askari zaidi ya 40 wakaanza kupambana na wabunge wa upinzani ambao walikua wamemzunguka mheshimiwa Mbowe,wakashikana mashati wakashindwa,askari wakaongezeka na kuongezeka wakamsihi wakashindwa,hatimaye Naibu spika akatoa amri ya kutumika nguvu kumtoa nje hapo ndio moto ukawaka na mwishoni askari wakafanikiwa kumtoa nje na wabunge wote wa upinzani wakatoka naye nje kasoro Mrema.
....nakuandalia habari ya Mrema alivyolamba matapishi yake leo......
0 comments:
Chapisha Maoni