| ||
|
ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA |
PASPORT YAKE |
HILO NDO BEGI MADAWA HAYO YALIKUWEMO |
AKIZITOA KWENYE MIKEBE YA POWDER NA SHAMPOO |
HUYO NDO ANTHONIA OJO AKIWA KITUO CHA POLISI |
MADAWA HAYO YAKIRUDISHWA KWENYE VYOMBO BAADA YA KUONESHWA KWA WANAHABARI. |
RECORD ZA ANTHONIA ALIWAHI KUJA TENA MWAKA 2011. |
Jitihada
za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na
waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda
baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na
kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.Anthonia
Ojo (25) Raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya baada ya
kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Dar es Salaam jana, akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa
ndege ya Ethiopian Airways. Msichana huyo aliingia hapa nchini Agosti 30
akitokea Nigeria. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege,
Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa
uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu
wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye
atafikisha mahakamani.
0 comments:
Chapisha Maoni