Searching...
Jumapili, 1 Septemba 2013

MTOTO MWENYE KICHWA KIKUBWA DUNIANI-HISTORIA YAKE INASIKITISHA

Hii ni picha ambayo inaweza ikawa ngumu kuiangalia lakini huyu ni binti mwenye umri wa miezi 18,sawa na mwaka mmoja na nusu ambaye historia yake inasikitisha sanaa!! 
Binti huyu ambaye amefahamika kwa jina moja la Roona amezaliwa maeneo ya ndani ndani sana katika kijiji kilichopo kaskazini mashariki mwa Indi.
"siku hadi siku kichwa chake kinakua na kuwa kikubwa,alikosa hamu ya kula na kulala muda wote,imetuwia vigumu sana kumbeba kwenda naye mahali popote" alisema baba yake Roona bwana Abdul Rehman.
Kichwa cha Roona kimekua na kufikia ukubwa wa mzunguko wa sentimita 94 mara tatu ya ukubwa wa mtoto wa kawaida'
Daktari aliyempima anasema kulikua na lita 10 za ziada za ute ute katika ubongo wake tatizo lililosababishwa na ama kuzalishwa kwa wingi kwa ute ute huo,mgandamizo au mapungufu ya kibaolojia ya kutokunyonywa kwa ute ute wa ubongo (cerebral fluid).

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!