Searching...
Jumapili, 1 Septemba 2013

AMWAGIWA MAJI YA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI KWENYE BIRTHDAY PART

Katika hali ya kuonyesha hisia za mapenzi binti mmoja mwenye umri wa miaka 19 mwanafunzi wa fani ya  Science Laboratory Technology (SLT) kitengo cha Osun State Polytechnic (OSPOLY) amekamatwa na polisi baada ya kumwagia maji ya moto mpenzi wake kisa wivu wa mapenzi.
Taarifa zinasema binti huyo alifanya kosa hilo jana usiku muda mfupi baada ya sherehe ya sikukuu ya kuzaliwa kwa kijana huyo zilizofanyika katika ukumbi wa Miracle jijini Lagos nchini Nigeria jana usiku.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Trust binti huyo aliyefahamika kwa jina la Yetunde alimwagia maji ya moto kijana Niyi Adelana kwasababu tu amewaalika wasichana na kusherehekea nao mbele yake.kijana Niyi anasoma diploma ya juu katika fani ya sayansi ya Computer kwa sasa ameelezwa kwamba na hali mbaya sana hosiptalini kufuatia kuunguzwa vibaya sehemu kubwa ya mwili na maji ya moto aliyomwagiwa na mpenzi wake Yetunde

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!