Searching...
Ijumaa, 13 Septemba 2013

FOLENI YA MALORI MPAKANI MWA TANZANIA MKOANI KAGERA ILIKUA BALAA.




Malori ya mizigo ya Tanzania yakiwa kwenye foleni eneo la Rusumo wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika mpaka wa Tanzania na Rwanda yakisubiri kukamilisha taratibu za kuingiza katika nchi hiyo jirani.
Kwa mujibu wa Maofisa wa Forodha katika mpaka huo upande wa Tanzania, kuanzia leo serikali ya Rwanda inatarajiwa kuongeza ushuru wa barabara kutoka dola za Marekani 152 hadi dola 500, hatua ambayo inadaiwa itasababisha usumbufu na hata foleni kubwa zaidi ya magari hayo kutokana na baadhi ya madereva kutokuwa na taarifa kuhusu ongezeko hilo ambapo wengi wao wanapewa  wanapewa na matajiri zao kiwango cha ushuru cha zamani.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!