
Sehemu ya msafara wa Mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiingia Shinyanga Mjini.

Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi
waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini .

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana
akizungumza na Meneja wa Kiwanda ya kutengeneza nguo na bidhaa
zitokanazo na pamba ya Dahong Textile Co.Ltd Jing Lin,kushoto ni Balozi
wa China nchini Lu Youqinq.

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana
akipata maelezo kuhusu uwekezaji kutoka China utakavyounufaisha mkoa wa
Shinyanga alipotembelea kiwanda cha Dahong Textile leo tarehe 13
Septemba 2013.

Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Dk.Ally Lufunga wakizungumzia fursa za mabadiliko ya viwanda
walipotembelea cha Dahong textile ambacho kitaleta mabadiliko makubwa
kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Sehemu ya Kiwanda cha Dahong Textile
kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi ,Kiwanda Hiki kitasaidia ajira
kwa watanzania zaidi ya elfu kumi na pia kitasaidia kupandisha uchumi
kwa wakulima wa pamba.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya Kiwanda cha Xing Hua Investment ltd Tina Mugisha ambaye amesema
kiwanda chake kitawezesha ajira nyingi na pia kuboresha bidhaa
zitokanazo na mifugo.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawekezaji wa viwanda kutoka
China mara baada ya kumaliza kuvitembelea viwanda hivyo,kushoto ni
Balozi wa China nchini Lu Younqinq.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini Lu Youqinq
wakiwapungia mkonno wajumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa,madiwani na
mabalozi wa nyumba kumi kwenye uwanja wa Kambarage.

Balozi wa China nchini Lu Youqinq
akisalimia wajjumbe wa halmashauri kuu ya mkoa ,madiwani na mabalozi wa
nyumba kumi katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga akipokea laptop kutoka kwa Balozi wa China Lu Youqinq.

Balozi
wa China nchini Lu Youqinq akimkabidhi laptop Katibu wa CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini Charles Charles katikati ni Mbunge wa Shinyanga mjini
Steven Masele.Picha na Adam Mzee
0 comments:
Chapisha Maoni