VICTOR MOSES
Katika hali ya kutaka kurejesha makali yake pamoja na heshima yake kwa mashabiki wake Liverpool wameamua kumwaga fedha katika usajili ili kukiimarisha kikosi chao kinachoongozwa na kocha wao Brendan Rodgers ambapo wametenga kitita cha paundi milioni 26 ili kuwanasa wakali watatu Victor Moses, Mamadou Sakho na Tiago Ilori dili ambalo linatakiwa kukamilika ndani ya saa 24 zijazo kabla dirisha la usajili kufungwa kesho saa sita usiku.
mshambuliaji wa Chelsea victor Moses anatarajiwa kujiunga na Liverpool kwa mkopo wa muda mrefu kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 1 ambapo taratibu zote za uhamisho wake zimekamilika kati ya Chelsea na Liverpool na kilichobaki sahivi ni yeye kukamilisha vipimo leo hii.
MAMADOU SAKHO.
Ukiachilia mbali Liverpool kumsajili mshambuliaji Moses pia wanataka kumsajili beki wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga na PSG Sakho kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 13 japokuwa wanapata upinzani kutoka kwa Arsenal ambao nao wanamtaka beki huyo.
Taarifa za uhakika zinasema tayari mchezaji huyo yupo makao makuu ya Liverpool Merseyside na anatarajiwa kumalizana na Liverpool leo na kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wao kwa mkataba wa miaka minne.
TIAGO ILORI.
Kufuatia dili la kumsajili TiagO Ilori kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 12 kukwama bado Liverpool wanaamini wanaweza wakafanikiwa kumsajili mchezaji huyo kutoka Sporting Lisbo.
0 comments:
Chapisha Maoni