Tajiri wa klabu ya Chelsea Mrusi Roman Abramovich katika hali ya kutaka kuiimarisha timu yake amejitosa kumpiga tafu kocha wake Jose Mourinho ambapo ameamua kuingia vitani kupambana na klabu ya Tottenham kwa kumpigia simu tajiri mwenzake wa Anzhi Makhachkala kumtaka amruhusu mchezaji wake ambaye William ajiunge na Chelsea badala ya Tottenham ambapo amekua chaguo lao baada ya kushindwa kuhimili mikiki mikiki ya kumbakisha mchezaji wao Gareth Bale kujiunga na Real Madri,kitendo ambacho kimemuudhi sana tajiri wa Tottenham.
TAJIRI WA KIRUSI NA MMILIKI WA KLABU YA CHELSEA ROMAN ABRAMOVICH
Bilionea huyo wa Kirusi na mmiliki wa klabu ya Chelsea Abramovich amempigia simu tajiri mrusi mmiliki wa Anzhi Makhachkala Oligarch Suleyman Kerimov na kumshawishi amuuzie mchezaji wake Willian kwa kitita cha paundi milioni 32.

Mchezaji huyo wa Brazil alitarajiwa kusaini jana alhamisi katika klabu ya Tottenham Spurs baada ya kufaulu vipimo vya afya lakini sasa imegeuka na kuwa ndoto baada ya Chelsea kuingilia kati usajili huo.
Tottenham
walikua na matumaini ya kuwasajili wachezaji wawili mbrazili huyo na mwingine kutoka Agentina Erik Lamela kama wachezaji mbadala baada ya Gareth Bale kuonekana kutimkia kunako Real Madrid
0 comments:
Chapisha Maoni