JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.
Kocha wa klabu ya Chelsea ya England amefunguka kwa kusema kwamba alikaribia kukubali kuifundisha timu ya taifa ya England mwaka 2007 lakini alikasema HAPANA kwasababu aliogopa kuboreka.
Shirikisho la soka la England FA walishikilia msimamo wao kwamba kocha Fabio
Capello ndiye alikua chaguo lao la kwanza kuchukua nafasi ya Steve McClaren, lakini
Mourinho amefunguka kwamba wakati huo alikua kwenye mazungumzo ya mwisho na FA na alikua karibu sana kuikubali kazi hiyo ya kuinoa timu ya taifa ya England.
‘Malengo yangu yalikua ni kujaribu kujipa moyo mwenyewe kukubali kazi hiyo ambayo hainiridhishi"alisema Mourinho.
‘nitakuwa nafanya nini siku ambazo sifundishi timu ya taifa? kwahiyo nitakuwa naenda kuwaangalia wachezaji wakifanya mazoezi kwenye vilabu vyao?kwahiyo nitawaruhusu makocha wangu wa magolikipa kufanya kazi nje ya timu ya taifa? natakiwa kufanya hivyo?
‘mwishoni mwa wiki ninaenda kuangalia mechi mbalimbali? hapana!! hapana!! ndio maana nikakataa kazi hiyo maana napenda kuwa karibu na wachezaji wakati wote!!alimalizia Jose amaourinho
0 comments:
Chapisha Maoni