Rais
Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji
wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya
dunia.
Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani.
Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote.
Rais
Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na
kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote
katika michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Sport Training Centre
(TSTF), Dennis Makoi amesema kuwa walipotambua kuwa kijana huyo
anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili
kukiendeleza. Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye
anamiliki
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa
katika kituo cha mfadhili huyo alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo
wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando,
Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka timu 44 kutoka nchi 14
ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye
kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa
kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo
ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni
kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza ambapo vijana
watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao na kuitangaza Tanzania.
Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa
malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo
Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.
0 comments:
Chapisha Maoni