Kocha wa Manchester United David Moyes anakabiliwa na uamuzi mgumu katika kipindi hiki ambapo anapaswa kuamua ama kuwaachia mashabiki uamuzi wa kumuhukumu katika mechi ya mwishoni mwa wiki hii kwenye mechi ya ngao ya hisani itakayopigwa katika uwanja wa kihistoria Wembley.
Taarifa zilizotolewa na klabu jumatatu kwamba Rooney hatakuwemo kwenye msafara wa kuelekea nchini Sweden kwenye mechi ya kirafiki itakayopigwa leo jumanne usiku kutokana na maumivu ya bega aliyoyapata katika mechi ya jumamosi iliyokuwa sio ya wazi,habari hizo zimezidi kuwaudhi mashabiki na kuongeza hali ya sintofahamu kutokana na msimamo wa nguli huyo kutaka kushinikiza kuondoka kujiunga na wapinzani wao Chelsea na mbaya zaidi ni kwamba Rooney ameshaweka wazi kwamba wiki hii ataandika barua rasmi ya kuitaka klabu yake imruhusu aondoke kwani amechoka maisha ndani ya klabu hiyo.
Habari njema kwa Man U ni kwamba nahodha wao aliyekua majeruhi amepona na leo atateremka dimbani,na katika hali ya kuonekana kutaka kumuachia Rooney klabu hiyo sasa ina mpango wa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Real Zaragoza Angelo Henriquez.
0 comments:
Chapisha Maoni