SAMWEL ETOO PHILS.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon ameonekana akishuka katika treni katika kituo cha train cha St Pancras akiongozana na wakala Pini Zahavi, akielekea kunako Chelsea mchana huu ili kukamilisha usajili wake wa kukipiga na matajiri hao wa London kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7,ambapo atakuwa analipwa kitita cha paundi 135,000 kwa wiki ikiwa ni zaidi ya nusu ya ule aliokuwa akilipwa kule Anzhi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amewahi kuchezea timu kubwa duniani kama Barcelona na Inter Milan mchana huu atafanyiwa vipimo vya afya kunako uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham complex kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
JOSE MOURINHO
Kocha wa klabu ya Chelsea mreno Jose Mourinho anaonekana kupumua baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya Etoo mchezaji ambaye aliwahi kufanya naye kazi kwa mafanikio makubwa walipokuwa wote Inter Millan.
DEMBA BA.
Wachambuzi wa soka wanchambua kwamba kitendo cha Etoo kutua Chelsea huenda ukawa mwisho wa mshambuliaji Demba Ba kunako Chelsea na huenda akarejea kwenye klabu yake ya zamani ya Newcastle kutokana na kocha wao kuonyesha nia ya kumrejesha nyumbani Ba ambaye amekua akikalia bench chini ya kocha Jose Mourinho.
Mshambuliaji wa Manchester United ambaye alionekana kuwa chaguo la kwanza la Jose Mourinho Wayne Rooney ameonekana kuamua kuendelea kukipiga na mashetani hao wa London Manchester United baada ya kuwa katika hali ya sintofahamu kuhusu maisha yake ya baadae baada ya kocha wake David Moyes kumchanganya kwa kumuambia kwamba yeye atakua mchezaji wa akiba akimsubiri Van Persie aumie ndio aingie
0 comments:
Chapisha Maoni