MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ataangalia
uwezekano wa kuhamia nje ya England, iwapo hatafanikiwa kuhamia Chelsea
majira haya ya joto.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United
anatarajiwa kuwasilisha barua ya maombi ya kuondoka wiki hii ili kutilia
mkazo wa ofa ya Pauni Milioni 30 kuhamia Stamford Bridge kujiunga na kocha mreno mwenye maneno mengi Jose Mourinho kocha ambaye amekua kipenzi cha Rooney kwa muda mrefu na anaona kama wakati sahihi sasa kutimiza ndoto yake.
Kocha wa Manchester United, David Moyes ambaye anaaminika kutaka
kumsajili kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, ameendelea na msimamo
wake akisema hadharani hatamuuza Rooney kwa klabu wapinzani wao wakuu
wa Ligi Kuu England.
Rooney na Chelsea kwa pamoja wanaendeela
kuamini kwamba United na kocha wao mpya, David Moyes watachemsha tu
kutokana na jinsi ambavyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaendelea kutilia mkazo suala la kuondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa
miaka tisa.
Ikiwa hawatamruhusu, Rooney ameamua bora kuhamia klabu nyingine itakayomvutia barani Ulaya kuliko kubaki Old Trafford.
Inafahamika kwamba Rooney hahofii
kuhamia popote, lakini atafurahi kwenda na mkewe Colleen na watoto
wao wawili wadogo katika timu ya Ulaya itakayotoa ofa nzuri, ili aondoke
Old Trafford.
Rooney Hakuwemo katika kikosi cha United
kilichokwenda kucheza na AIK Stockholm nchini Sweden jana kujiandaa na
msimu, kutokana na maumivu ya bega na Rooney anatarajiwa kupona maumivu
hayo aliyoyapata mazoezini mwishoni mwa wiki. Anaweza kuwa tayari kwa
safari ya Wembley ambako Moyes atapeleka kikosi chake kwania Ngao ya
Jamii dhidi ya Wigan Jumapili.
Marouane Fellaini, akifanya mazoezi na Everton jana, anaweza kuhamia Manchester United kujiunga na kocha wake wa zamani Moyes kama mbadala wa Cesc Fabregas anayeonekana kung'ang'aniwa na Barcelona.
0 comments:
Chapisha Maoni