Searching...
Jumatano, 7 Agosti 2013

UWANJA WA NDEGE NAIROBI WAWAKA MOTO-SAFARI ZAFUNGWA,WASAFIRI WAHAHA,ANGA YAFUNGWA KWA MUDA


Moto ukiungua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya.
MOTO mkali umezuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya asubuhi hii hali iliyopelekea mamlaka ya uwanja huo kuufunga kwa muda ili kukabiliana na hali hiyo. Safari zote za ndege zinazotumia uwanja huo kwa sasa zimesitishwa na ndege zote ambazo zilikuwa zitue katika uwanja huo kwa sasa zimeelekezwa katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Moi, Mombasa na Kisumu.
Chanzo cha moto huo mpaka sasa bado hakijafahamika. Mamlaka ya uwanja huo yamedai kuwa mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika moto huo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!