Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S.L. Utouh.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S.L. Utouh
amekutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam ambapo ametoa ufafanuzi kukanusha tuhuma zilizotolewa
kupitia baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
PAC kwamba, kuna ufisadi katika matumizi ya fedha zilizotolewa katika
bajeti ya 2011/2012 kwa ajili ya mradi maalum wa barabara unaosimamiwa
na Wizara ya Ujenzi.
Bw.
Utouh amebainisha kwamba kiasi cha Shs. 252,975,000,000.00
kilichohojiwa katika ukaguzi, ni fedha ambazo zimeonyeshwa kwenye
taarifa za hesabu za Wizara kama ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012
tofauti na uhalisia wenyewe ulivyo.
Serikali
katika dhamira ya kuimarisha mtandao wa barabara nchini, iliweka kwenye
bajeti yake ya mwaka wa fedha 2011/12 Kasma maalum ya ujenzi wa miradi
ya barabara na kuitengea jumla ya shilingi 252,975,000,000.00 kwa ajili
ya kulipia kazi za barabara zinazoendelea.
Fedha
zote zilitolewa na HAZINA kwa madhumuni hayo na kwa kufuata taratibu za
Serikali. Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS ililipia kazi hizo za
barabara kwa maana ya madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri wa
miradi mbalimbali inayoendelea.
“Hivyo
katika kujadili hesabu za Wizara ya Ujenzi hakukuwepo tuhuma zozote za
ufisadi. Katika majadiliano yake Kamati ya Bunge ilimtaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuihakikishia kamati hiyo matumizi ya
fedha hizo, jambo ambalo litafanyika” alielezea Bw. Utouh.
Bw.
Utouh ameviasa vyombo vya habari kuepuka kutumia nukuu zenye lengo la
kuchonganisha jamii na hasa zinazolenga kupotosha ukweli wa jambo lililo
katika taratibu rasmi za majadiliano.
Katika
hatua nyingine CAG Bw, Utouh alichukua fursa hiyo kuipongeza Wizara ya
Ujenzi kwa kazi nzuri sana inayofanya ya kusimamia na kujenga barabara
katika kona zote za nchi yetu. “Tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya
ili wawe na moyo wa kuchapakazi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu”
alisistiza Bw. Utouh.
0 comments:
Chapisha Maoni