Msaidizi
wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi
Kayanda, akimkabidhi Pikipiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geordan
Rugimbana, aliyeikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe
pande kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi iliyofanyika
leo katika mji huo mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa
Mabwe Pande, Abdallah Kunja.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Geordan Rugimbana, akimkabidhi Pikipiki na
nyaraka muhimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande,
Abdallah Kunja, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo
mpya, ambapo Mkuu wa Wilaya, aliikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa
Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais.
Sehemu ya wakazi wa Mji Mpya wa Mabwe Pande waliohudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo
baada ya makabidhiano.
Picha na OMR
0 comments:
Chapisha Maoni