RAIS Jakaya Kikwete amemuomba
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Yoweri Museveni wa
Uganda, kuwa msuluhishi wa mgogoro wa chini kwa chini unaoendelea kati
ya Tanzania na Rwanda.
Uamuzi huo, ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pinda alitangaza uamuzi huo, wakati
akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambapo Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alitaka kujua hatua za
Serikali katika kile kinachoonekana Tanzania kutaka kutengwa katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbowe, alisema hatua ya nchi za
Rwanda, Kenya na Uganda kuendesha vikao kupitia wakuu wa nchi ikiwemo
kujitoa kwa nchi ya Rwanda kutumia Bandari ya Dar es Salaam, kunaashiria
mwelekeo mbaya.
0 comments:
Chapisha Maoni