Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na viongozi wa Jeshi la
Polisi, Jeshi la Wananchi, Marekani pamoja na waandishi wa habari kabla ya
kuzindua mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la
Polisi na Jeshi la Wananchi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya
Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio
hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa
yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo
umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam
leo.
|
0 comments:
Chapisha Maoni