Timu ya taifa ya England ya mpira wa Cricket imelazimika kuomba radhi kutokana na shutuma za wachezaji wa timu yao kukojolea uwanjani wakati wakisherehekea ushindi wa 3-0 dhidi ya timu ya Ashes
‘Timu ya taifa ya cricket ya Englandinapenda kuweka wazi kwamba wakati tukisherehekea ushindi wetu dhidi ya Ashes hatukuwa na kusudio lolote la kukojolea uwanjani na tunataka ifahamike kwamba Cricket ni mchezo tunaoupenda sana,’ilisomeka taarifa ya timu hiyo.
‘Sisi kama timu tunajivunia wenyewe jinsi tunavyoheshimu vitu vyote vya mchezo huu wa cricket
ikiwemo timu pinzani na uwanja tunaochezea pia.
‘Lakini tunapenda kuweka wazi kwamba kama kuna mtu yoyote amekwazika na tukio hilo tunaomba radhi na tunataka kuwahakikishia kwamba hilo lilikuwa ni tatizo dogo ambalo halitajirudia tena.’ilimalizia taarifa ya timu hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni