Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mfanyibiashara maarufu jijini arusha anayemiliki migodi kadhaa ya madini ya Tanzanite na Hoteli za kitalii Bwana Erasto Msuya amefariki dunia mchana wa leo baada ya kupigwa risasi nyingi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kisha kufariki dunia hapo hapo.
akizungumza na mtandao huu wa MCHOME BLOG Kamanda wa polisi mkoani kilimanjarao ROBERT BOAZ amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Bwana Erasto alikua njiani kuelekea Moshi akitokea arusha ambapo alipofika maeneo ya njia panda ya KIA alisimamishwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi lakini ikionekana kama wanafahamiana kwani walichukua muda kidogo kujadili mambo ambayo hayajajulikana na kisha walionekana kushindwa kuelewana ndipo watu hao walipommiminia risasi nyingi ambazo kamanda wa polisi ROBERT BOAZ amesema ni risasi nyingi ambazo haijafahamika idadi yake.
"Amepigwa risasi nyingi sana,bado hatujajua idadi kamili ya risasi alizopigwa....na katika eneo la tukio tumeokota maganda ya risasi zinazotumika katika bunduki ya kivita ya SMG" kamanda wa polisi mkoani kilimanjaro aliiambia MCHOME BLOG muda mfupi uliopita.
Taarifa zaidiza tukio hili zitakujia muda sio mrefu
MUNGU AILAZE MAHALA PEMA ROHO YA ERASTO MSUYA AMEEEN!!
0 comments:
Chapisha Maoni