Na Edwin Moshi, kilimanjaro
Imeelezwa
kuwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mzuri na viongozi
wa serikali kuanzia ngazi ya chini ni moja ya mafanikio yanaolifanya
shirika la TUSONGE kuelekweka kwa wananchi wanaofanya nao kazi
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la TUSONGE lililopo Moshi mkoani
Kilimanjaro Bi. Aginatha Rutazaa (aliyesimama pichani) wakati
akizungumza na wafanyakazi wa shirika la SUMASESU lililopo wilayani
Makete mkoani Njombe lilipofanya ziara katika shirika hilo yenye lengo
la kubadilishana mawazo na kujifunza mbinu mbalimbali wanazozitumia
kufikisha ujumbe kwa jamii
Bi
Aginatha amesema wakati wa ufanyajikazi katika shirika lake wamekuwa
wakishirikiana kwa pamoja na wananchi pamoja na viongozi wa serikali
ikiwemo mitaa na vijiji ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wenye watu na
ukiwashirikisha ni rahisi ujumbe kufika kwa jamii
Shirika
hilo ambalo linatoa elimu ya mambo mbalimbali kwa wananchi ikiwemo
UKIMWI na ujasiriamali, limefanikiwa kuanzisha vikundi vya kuweka na
kukopa kwa wajasiriamali wadogo ( wa hali ya chini) ambapo walipata
wasaa wa kutembelea kikundi kimojawapo kilichopo kata ya Karanga na
kujionea kinavyofanya kazi
Pia
amesema wanatumia video kuonesha elimu mbalimbali hasa magonjwa ya
ngono na UKIMWI ili ujumbe ufike moja kwa moja kwa jamii na kuona hali
halisi ya kile kinachozungumziwa
Kwa
upande wake mkurugenzi wa SUMASESU Egnatio Mtawa alishukuru kwa
mapokezi mazuri ya shirika la TUSONGE ambapo pamoja na mambo mengine
alikiri kujifunza mengi mazuri kutoka kwao na kuahidi kwenda kuyatumia
kwenye shirika lake ili jamii iweze kusonga mbele
0 comments:
Chapisha Maoni