Searching...
Jumamosi, 20 Julai 2013

TAARIFA YA IKULU: RAISI KIKWETE AKUTANA NA PROF. IBRAHIM LIPUMBA...!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete akutana na Profesa Lipumba
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Alhamisi, Julai 18, 2013, alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.
      Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala ya kitaifa na jinsi gani wadau mbali mbali wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

19 Julai, 2013

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!