Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na viongozi wengine pamoja na watumishi
wa serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru
uliowasi
li Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani
Katavi.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Alhaj Salum Mohammed Chima na viongozi wengine pamoja na watumishi wa
serikali ya Mkoa huo wakishangilia mapokezi ya mwenge wa uhuru
uliowasili Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 19 Julai 2013, ukitokea Mkoani
Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya mapema leo tarehe 19 Julai 2013,
baada ya mwenge huo kumaliza ziara yake Mkoani Katavi na kuanza ziara ya
siku nne Mkoani Rukwa.
Kiongozi wa mbio za
mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizindua mradi wa maji katika
kijiji cha Challa B leo tarehe 19 Julai 2013. Mwenge wa Uhuru umeanza
ziara yake ya siku nne Mkoani Rukwa kwa kuanzia na Wilaya ya Nkasi na
kuendelea Kalambo na Sumbawanga.
Baadhi ya watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.





0 comments:
Chapisha Maoni