Searching...
Alhamisi, 11 Julai 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



SAKATA LA ONGEZEKO LA KODI YA SHILINGI 1000 MOAT HAWAKUHUSISHWA

 Mchakato wa kupitisha ongezeko la kodi ya Shilingi 1,000 kwa kila mtumiaji wa simu kwa mwezi uliotokana na mabadiliko ya muswada wa fedha  wa mwaka 2013 na kupitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania haukushirikisha Chama cha Makampuni ya Simu za Mkononi (MOAT).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoletolewa kwa vyombo vya habari na MOAT, imeeleza kuwa Chama hicho cha Makampuni ya Simu kilikutana na Kamati ya Bajeti ya Bunge ili kupata usahihi wa maana ya huduma za mawasiliano ya simu kama ilivyoainishwa katika muswada wa mwaka 2013.
Katika kikao hicho, mawasiliano ya simu yalitafsiriwa kuwa ni huduma yoyote inayotolewa na Kampuni ya mawasiliano ya simu kwa kutuma, kupokea mawimbi, maneno, picha na sauti au habari ya aina yoyote kwa kutumia mfumo wa kielektronikia wa picha au mfumo mwingine wowote.
Sisi kama waendeshaji wa mitandao ya simu hatukushirikishwa katika kujadili mfumo huu mpya wa   kulipa kodi ya Shilingi 1,000 kwa kila laini. Tunaiomba serikali iliangalie upya sulala hili la ushuru huo ambapo kwa kufanya hivyo watawezeshe ukuaji wa mawasiliano ya simu nchini Tanzania. Ukuaji wa mawasilaino ya simu nchini Tanzania unaridhisha ambapo takwimmu zinaonesha ukuaji huo ni asilimia 48, kiasi ambacho ni sawa na watu takribani milioni 22 ambapo kati yao watu  milioni 8 hutumia chini ya Shilingi 1,000 kwa mwezi kwa mawasiliano ya simu.
Taarifa hiyo ya MOAT imeeleza kuwa inatambua jitihada za serikali katika kukusanya kodi kwa ajili ya mipango ya maendeleo kwa wananchi, Hata hivyo MOAT imebainisha kuwa kuanzishwa kwa kodi hiyo kunakinzana na juhudi za kuwapunguzia mizigo ya kodi wananchi wenye kipato cha chini.
Chama hicho kimesema kuwa ukuaji wa mawasiliano ya simu katika muongo ujao utatoka maeneo ya vijijini, hata hivyo, taarifa hiyo imeeleza kwamba uanzishwaji wa kodi mpya ya Shilingi 1, 000 kwa kila mtumiaji wa simu kila mwezi utazuia juhudi zaidi za ukuaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini kwasababu watu wengi ambao ni wenye kipato cha chini hawataweza kutumia mawasiliano huduma hiyo.
"Ulipaji wa kodi mpya ya shilingi 1, 000 kwa kila mtumiaji wa simu kwa mwezi udhoofisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mawasiliano ya simu hadi hivi leo, ambapo tumeshuhudia huduma hiyo imezidi kuwa nafuu kwa ajili ya wote," anasema Chama.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!