Man City wameamua kuvunja Bank ili kutoa kitita kikubwa ambacho kitaweza kuwashawishi Real Madrid pamoja na Ronaldo mwenyewe kutua Etihad msimu ujao wa ligi kuu England
Habari za neema zaidi kwa Ronaldo zinasema Man City wamemuambia wakala wa Ronaldo kwamba wapo tayari wamejiandaa kumlipa kiasi chochote cha fedha zaidi ya kile alichoahidiwa na Man U kwa maana kwamba wanaweza kumlipa zaidi ya paundi laki tatu kwa wiki
Manchester United wamejitahidi kwa takribani miezi mitano iliyopita kumrudisha mshambuliaji huyo bila mafanikio lakini wao City wameamua kuvunja bank ili kumvutia Ronaldo.
Ronaldo bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Madrid
Mkurugenzi mtendaji na mkurugenzi wa ufundi wa Man City wamemuambia wakala wa Ronaldo kwamba wapo tayari kufanya lolote muda wowote,
Kocha wa zamani wa Man U Sir Alex Ferguson ndiye aliyemuibua na kumfanya mchezaji bora duniani ambapo mpaka sasa United wapo tayari kurudisha paundi milioni 70 kwa Madrid ili kumrejesha Old Trafod lakini wakala wa Ronaldo amesema itakuwa ni vigumu sana kwa Madrid kukataa ofa ya Man City kwani ni kitita kikubwa sana.
0 comments:
Chapisha Maoni