Searching...
Jumatano, 17 Julai 2013

SERIKALI KUCHUNGUZA VIKWAZO VYA UBANGUAJI WA KOROSHO

 Wafanyakazi wa kiwanda cha Korosho Africa wakiwa kazini
Korosho ikiwa imetengwa kwa daraja la "A" baada ya kuchambuliwa
-----------------------------------------
Na Steven Augustino, Tunduru
SERIKALI imeahidi kufanya uchunguzi wa kina katika Viwanda vyote 10 vilivyo jengwa kwa ajili ya kubangulia Korosho za Wakulima nchini zikiwa ni juhudi za kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kero ya kukosekana kwa soko la uhakika la zao hilo.

Sambamba na ahadi hiyo ya serikali pia imewahakikishia Wakulima hao wa Korosho kote nchini kuwa itatoa fedha katika kipindi cha miezi miwiIi ijayo ikiwa ni muda mfupi baada ya utafiti huo ili kuviwezesha viwanda hivyo kununuaa mitambo mipya zikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha kuwa zao hilo linaapata soko la uhakika. 
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na Serikali kuchunguza kwa kina changamoto hiyo inahitaji hitaji ufumbuzi wa kudumu ili kuwaletea maendeleo ya kweli wakulima wake. 
Alisema hali hiyo imetokana na Serikali kubaini kuwa utaratibu wa kutumia Staakabadhi ghalani ambao ulibiniwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa zao hilo katika awamu tatu kuto onesha mafanikio na hata ukiachwa uendelee kwa muda mrefu hautawaletea tija wakulima hao.
Aidha katika hotuba hiyo pia Waziri pinda akaeleza kuwa katika kuonesha kuwa maamuzi hayo siyo nguvu ya soda alisema kuwa pia Serikali imejipanga kutoa fedha katika viwanda hivyo na kuviwezesha kununua vyenyewe Korosho kutoka kwa wakulima ili kukata mirija ya unyonyaji kwa kuwaondoa wakulima hao katika mikono ya wanyonyaji. 
Katikaa taarifa hiyo Waziri Pinda alisema kuwa kutokana na hali hiyo tayari Serikali imekwisha unda kikosi kazi cha watu 5 kitakachosimamiwa na Katibu mkuu wa Ofisi yake na kwamba kazi ya kwanza itakuwa ni kupita katika viwanda hivyo hata kama vimeuzwa na kuchunguza kwa kina matatizo yanayo vikwamisha aviwanda hiovyo kuendeleaa na kazi iliyo kusudiwa wakati wa ujenzi wake.
Huku akishangiliwa na maaelufu waliojitokeza kusikiliza mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tunduru Mjini Mtoto wa Mkulima aliendelea kubainisha kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi hilo serikali itaanda utaratibu wa kutoaa fedha katika kipindi cha miezi miwili ijayo zitakazo visaidia kununua mitambo mipya na kuanza kazi ya ubanguaji wa Korosho za wakulima mara moja.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ameondoka Wilayani Tunduru kuendelea Ziara yake Wilayani Namtumbo Mkoani humo.  


0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!