Bi. Jacqueline Mkindi mkurugenzi
mkuu wa TAHA akiwakaribisha Mh. Rajab Mbarouk Mohammed na Mh. Murtaza Ally
Mangungu walipowasili katika ofisi za Tanzania Horticultural Association (TAHA)
kwa ajili ya kupata maelezo ya awali kuhusu hali halisi ya maendeleo ya
Horticulture nchini Tanzania.
Bi.
Jacqueline Mkindi akiwasilisha
maelezo ya awali kuhusu maaendeleo ya Horticulture nchini Tanzania kabla
ya wabunge kwenda kutembelea baadhi ya mashamba ya horticulture
yanayoendeshwa na
kumilikiwa na wakulima wanachama wa TAHA.
Wabunge wakiangalia kitalu cha shamba la Arusha Blooms
kilichopandwa maharage machanga ambayo huzalishwa na kuuzwa katika masoko
makubwa yaliyo ndani na nje ya nchi, maharage hayo hutumika katika chakula kama
mboga.
1. Moja ya vitalu vya maharage
machanga kwenye shamba la Arusha Blooms
Msimamizi wa kitalu cha maharage
machanga, Masawe akitoa maelezo ya teknolojia inayotumika katika kuzalisha
mazao ya horticulture shambani hapo.
Wabunge wakiangalia Jembe la kulimia linalokokotwa na
trekta ambalo limebuniwa na kutengenezwa kwa gharama nafuu hapa hapa nchini
Tanzania.
Mh. Mahamoud Hassan Mgimwa akiangalia namna ambavyo
maharage machanga yamehifadhiwa kwenye pakiti maalumu ambayo hutumika
kusafirishia bidhaa ya mazao hayo katika masoko makubwa nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Mashamba ya Rijk Zwaan Afrisem Ltd,
Heikki Niskala akifafanua jambo kwa wabunge wakati timu ujumbe wa wabunge
ulipofika katika ofisi za mashamba hayo kama sehemu ya ziara yao ya kilimo
Mkoani Arusha.
Awali,
Wabunge walipokewa na Wajumbe wa bodi na baadhi ya wafanyakazi kutoka
Sekretarieti ya TAHA ambapo walikaribisha na kushiriki kwa pamoja katika
chakula cha jioni.
Sehemu ya matunda yaliyopendezesha chakula cha jioni siku hiyo.
Wakurugenzi kutoka bodi ya TAHA, kulia ni ndugu Juma Lossini akisalimiana na Bi. Fatma Riyami
Timu ya TAHA ikiteta jambo na Mh. Jitu Vrajlal Soni (hayupo pichani)
Mh. Mahamoud
Hassan Mgimwa akimsikiliza Mkurugenzi wa TAHA kwa umakini wakati wa
chakula cha jioni ndani ya hotel ya Mount Meru Arusha.
Wabunge kutoka kamati mbalimbali za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wafanyakazi kutoka Wizara ya
Kilimo, Chakula na ushirika wamefanya ziara ya kilimo ambayo pia iliwafikisha
kwa wakulima na wanachama wa taasisi ya Tanzania Horticultural Association
(TAHA), TAHA ni taasisi kilele inayoundwa na wanachama wakulima wa kilimo cha
mazao ya horticulture nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo wabunge walipata
fursa ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa bodi na secretariat ya TAHA ambayo
iliainisha changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wakulima wanachama
wa TAHA katika shughuli zao za kila
siku. Tazama taswira ya ziara ya wabunge
hapa.









0 comments:
Chapisha Maoni