Home
»
Unlabelled
» ROONEY SI LOLOTE SI CHOCHOTE-ASEMA DAVID MOYES
WAYNE ROONEY.
Wayne Rooney anakabiliwa na maisha magumu sana ya kusugua benchi kama ambavyo kocha mpya wa Manchester United David Moyes alivyomuambia Rooney kwamba hayupo kwenye kikosi chake cha kwanza kwani chaguo la kocha huyo kwa mshambuliaji namba moja ni Robin van Persie hivyo itamlazimu kuanzia Benchini ambapo katika hali ya kummaliza kabisa Rooney,Moyes amesisitiza kwamba Shinji Kagawa ndiye chaguo lake la kwanza kucheza nyuma ya Van Persie,kauli ambayo imemfanya Rooney kuhisi ndio amepewa ruhusa ya kufungasha viragi vyake man u.
ROBIN VAN PERSIE.
Kwa sababu hiyo ya kukaa bench kumsubiri Van Persie aumie ndio acheze sasa Rooney analazimika kuangalia klabu ambayo itamhakikishia kucheza timu ya kwanza japo Moyes amesisitiza kwamba Rooney Hataondoka kwani ndiye mchezaji wa kuchukua nafasi ya Van Persie akiumia kitendo ambacho Rooney amechukulia kama kejeli kwake ambapo amesema hawezi kukaa klabuni hapo kama mchezaji wa akiba ROONEY NA EVRA.
Matthew Peters
Kutokana na msukumo mkubwa wa Chelsea kutaka kutoa kitita cha paundi milioni 40 kumng'oa Rooney Manchester United kunaweza kukamlazimisha Moyes kumuachia Rooney aondoke zake baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka nane. “Yote kwa yote malengo yangu kwa Wayne Rooney ni kwamba kwa lolote litakalomtokea Robin van Persie kama vile kuumia, basi tutamhitaji Rooney” alisema Moyes. “Manchester United sio kwaajili ya Wayne Rooney. Manchester United ni kwaajili ya timu nzima. “sitakuwa tayari kumruhusu Wayne Rooney kuwa mtu muhimu kuliko klabu yenyewe na timu zima kwa ujumla kamwe haitawezekana”
WAYNE ROONEY NA MKEWE COLEEN.
Vile vile Moyes
amesema United hawatampa ofa ya mkataba mwingine Rooney, ambaye bada ana mkataba wa miaka miwili unaompa mshahara wa paundi 250,000 kwa wiki.Rooney
amerejea nyumbani na kuiacha timu huko Bangkok ikiendelea na maandalizi ya msimu ujao baada ya kuumia ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu.
DAVID BECKHAM. David Beckham amesema anayo matumaini makubwa kwamba Wayne Rooney ataendelea kukipiga na mabingwa hao bila kujali sintofahamu inayojitokeza kwa maisha ya baadae ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.
0 comments:
Chapisha Maoni