Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imeizidi kete Manchester United baada ya kufanikisha mipango yao waliyokuwa wanaifanya kimya kimya ya kumsainisha mchezaji wa Barcelona Thiago Alcantara kwa kitita cha paundi milioni 21.6.
Kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22,sasa atajiunga tena na aliyekuwa kocha wake Pep Guardiola ambaye sasa anawafundisha mabingwa hao wa Ulaya na Ujerumani Bayern Munich.
"Thiago Alcantara alikuwa na hamu kubwa sana ya kujiunga na kocha Pep Guardiola," alisema mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge.
Mabingwa hao wa Ujerumani na Ulaya wamesema Thiago anatarajiwa kukamilisha vipimo vya afya Munich wiki hii kabla ya kusaini mkataba mrefu wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka minne.
0 comments:
Chapisha Maoni