Searching...
Jumatatu, 15 Julai 2013

BAADA YA KUMKOSA THIAGO MAN U SASA KUHAMISHIA MAJESHI KWA FABREGAS

United target Fabregas after Thiago snub
CESC FABREGAS.
Baada ya Manchester United kumkosa kiungo wa Barcelona Thiago Alcantara baada ya kutimkia Bayern Munich sasa kocha wa Man U David Moyes amesema anaelekeza nguvu zake kumng'oa kiungo wa mwingine wa Barcelona Cesc Fabregas.
Taarifa za uhakika kwamba United wamemkosa kiungo huyo wa kimataifa Thiago Alcantara zilitangazwa jana na Barcelona kwamba wamemuuza mchezaji huyo kwa Bayern Munich kwa dau la paundi milioni 21.6.
uwezekano wa United kumpata Fabregas ni mdogo kwani kiungo huyo wa zamani wa Arsenal amesema anafurahia maisha Barcelona na anataka kuendelea kuchezea klabu hiyo ya hispania
Man U wanaamini wanaweza wakampata kiungo huyo mwenye miaka 26 ambaye anafanya kila liwezekanalo na kuongeza juhudi ili kupata nafasi ya kikosi cha kwanza Nou Camp hasa baada ya ujio wa mbrazil Neymar.
Frustrated: Fabregas has found starts limited at Barcelona (Picture: Getty Images)

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!