Mchezaji Wayne Rooney alitarajiwa kuwasilisha rasmi ombi la kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya kuwaambia viongozi wake kwamba amekerwa sana na kauli aliyoitoa kocha wake David Moyes, kwamba kwa malengo yake(kocha) msimu ujao ni kumchezesha timu ya pili kama mbadala wa Van Persie na atacheza endapo tu Van Magoli ataumia vinginevyo atakalia bench mwanzo mwisho.
JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, aliiongezea ukakasi kauli ya Moyes baada ya kusema kwamba kama Rooney ni mchezaji wa kikosi cha pili au mchezaji wa akiba wa Man United, basi ni dhahiri kwamba hawezi kuitwa kwenye timu yake ya taifa.
Habari za ndani kutoka kwa Rooney mwenyewe zinasema mchezaji huyo anajiamini kwamba yupo kwenye kiwango cha juu tofauti sana na jinsi wanavyomdhalilisha,na kwamba hayupo tayari kuruhusu kuporomoka kiwango chake kwa kuchezeshwa kikosi cha akiba “Rooney haamini kwamba kuna lolote ambalo anaweza kulipata kuongeza kiwango chake kama mchezaji wa akiba ukilinganisha na mafanikio makubwa aliyoyapata miaka tisa akiwa na klabu hiyo”alikaririwa rafiki yake wa karibu
DAVID MOYES - KOCHA MAN U.
mwishoni mwa wiki Moyes
alisema kwamba “Ninaweza nikampanga Rooney endapo tu Robin Van Persie ataumia na sio vinginevyo”
Rooney
atapaswa kuwasilisha maombi rasmi ya kwamba anataka kuondoka “nafikiri hamunielewi,sijui nimeongea lugha tofauti,narudia tena na tena...Rooney hauzwi” alisema Moyes wiki iliyopita baada ya kauli ya Mourinho kutoa kauli ya kuonyesha Rooney atatua Chelsea.
0 comments:
Chapisha Maoni