Searching...
Jumanne, 23 Julai 2013

NAOGOPA TIMU KUFANYA VIBAYA-DAVID MOYES AANZA VISINGIZIO

Moyes reveals 'fear' of United jobDAVID MOYES
Kocha wa Manchester United David Moyes ameanza kuonyesha dalili za kushindwa kuendeleza gurudumu la mafanikio yaliyoachwa na mzee muheshimiwa sana ndani ya Manchester United japo amesema anaimani atapata mafanikio ndani ya Old Trafford.
Moyes yupo kwenye maandalizi ya kuiongoza Man u kwa mara ya kwanza baada ya kuirithi mikoba ya mzee Sir Alex Ferguson katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
kocha huyo wa zamani wa Evertonakiwa katika shinikizo la kupata matokeo mazuri kwa haraka kama mashabiki wake wanavyotarajia kuendeleza ubabe kama alivyoacha Ferguson kitu ambacho amekiri sio kirahisi hata kidogo.
‘Ni lazima uwe na chembe chembe za uoga katika majukumu mazito ya kukiongoza klabu kikubwa duniani kama Manchester United, Moyes aliliambia gazeti la Daily Mail.
‘inakufanya ufanye kazi zaidi,inakulazimu uone mbali zaidi na inakusaidia kujaribu na sio macho yako kuangalia nje ya mpira.
‘Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema kuiongoza  Manchester United ni kitu kirahisi ila ni changamoto..
"Lazima niwe wazi,mafanikio ya Manchester United ni kama kufanya biashara msimu wa usajili na ukashindwa wakati wa ligi maana nimeshindwa kuwapata wachezaji wote niliowatarajia kama Cesc Fabregas,Thiago Alcantara na Leighton Baines,lakini hii ndiyo timu yangu,lazima niwajibike alimalizia Moyes huku akiwa katika uso wa huzuni”.’
Singha All Star XI v Manchester United

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!