Searching...
Jumatatu, 22 Julai 2013

MILELE HUWEZI KUMLINGANISHA LUKAKU NA DROGBA-MOURINYO



Jose: Lukaku's no Drogba but he can dislodge Torres
ROMELU  LUKAKU
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema anaamini Romelu Lukaku anaweza kuleta changamoto na ushandani na Fernando Torres kwenye ligi kuu laki kamwe huwezi kumlinganisha huyu kijana mdogo wa Ubelgiji na mkongwe Didier Drogba.
Lukaku tayari amefunga magoli mawili katika ziara yao huko mashariki ya kati na kumvutia mreno kocha Jose Mourinho kumrejesha Stamford Bridge.
Torres bado yupo likizo ndefu baada ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Hispania kwenye kombe la Confederations huko Brazil ambapo katika mechi yao ya fainali walifungwa magoli matatu kwa bila na Brazil.
Romelo Lukaku ambaye alikua na msimu wa mafanikio katika klabu ya West Brom sasa anafanya kila awezalo kuhakikisha anarejea nyumbani Chelsea.
Chelsea Coach Jose Mourinho (L) shares a joke with striker Didier Drogba  during Chelsea training and press conference ahead of tomorrow's Champions League Quarter Final Second Leg match against Valencia, at the Stadium Mestalla on April 9, 2007 in Valencia, Spain.  (Photo by Stu Forster/Getty Images)
MOURINHO NA DROGBA.
Mourinho akaongeza kuwa ,"kijana ni mchezaji mzuri,hilo halina ubishi maana anaweza akaleta ushindani na  Torres,amejifunza kucheza mchezo ninaouhitaji"alisisitiza Mourinho.
‘kila kocha anakuwa na mfumo wake,Lukaku alikua na kocha mzuri sana msimu uliopita,lakini Steve Clarke atabaki kuwa Steve Clarke, na mimi nitabaku kuwa Mourinho, na West Brom sio Chelsea.
‘ni juu ya kijana mwenyewe,lakini ni muwazi na muelewa kile tunachokitaka.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!