Searching...
Jumanne, 16 Julai 2013

LAZIMA ROONEY NA BENTEKE WATUE CHELSEA-HAZARD

Hazard: Blues should buy Rooney and Benteke
EDEN HAZARD.
Sinema ya Rooney ikiwa inaelekea ukingoni baada ya steling msaidizi wa sinema hii David Moyes kuonekana kuishiwa mbinu za mpambano sasa mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Chelsea Eden Hazard ameingia katika sinema hiyo akimshawishi kocha wao mreno Jose Mourinho kuhakikisha anawanyakua washambuliaji nguli Wayne Rooney na Christian Benteke ili watue Stamford Bridge msimu ujao.
Boss wa the Blues Mourinho yupo katika mawindo makali ya washambuliaji wa kuimarisha kikosi chake msimu ujao akiwa tayari ameshawakosa washambuliaji wawili ambao walionekana kuwa chaguo lake la kwanza Edinson Cavani na Robert Lewandowski.
FBL-THA-ASIA-ENG-PR-MANUTD-FILES
WAYNE ROONEY.
‘Rooney atakuwa amefanya chaguo zuri sana akisaini Chelsea,’ alisema Hazard.
‘ni mchezaji mkubwa mwenye uzoefu wa kutosha na bado ni kijana mdogo wa umri wa miaka 27.
‘naamini atafanya vizuri hapa Chelsea"alimalizia Hazard.
FBL-WC2014-BEL-TRAINING
CHRISTIAN BENTEKE.
Lakini Hazard hakuishia kwa Rooney tu,alienda mbali zaidi ambapo alimpendekeza mchezaji wa Aston Villa  Benteke.
‘amekuwa na msimu wa kwanza mzuri sana kama mshambuliaji bora mdogo ligi kuu ya England.
‘Ndoto zake ni kucheza vizuri zaidi,nafikiri atakuwa na mchango mkubwa sana katika klabu kubwa kama Chelsea’
Chelsea wapo kwenye mkakati wa kuwapata wote wawili  Rooney na Benteke, japo kuna taarifa kwamba mpango wa klabu ni kununua mshambuliaji mmoja tu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!