Searching...
Jumanne, 16 Julai 2013

MAN CITY WALAMBA DUME-ARSENAL WAENDELEA KUSAJILI KUPITIA MAGAZETINI

Jovetic close to £25m City switch
STEVAN JOVETIC
Manchester City wanayo matumaini makubwa kumalizana na mchezaji Stevan Jovetic wiki hii baada ya kuripotiwa Man City kukubaliana na klabu ya Fiorentina ada ya uhamisho ya paundi milioni 25
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Montenegro hapo awali aliripotiwa kutua Arsenal mwanzoni mwa uhamisho ulipoanza lakini kitita kikubwa kilichowekwa mezani na Man City kikazifanya klabu zingine zilizokuwa zinammezea mate za Juventus na Chelsea kuishia kunawa.
Kocha mpya wa Man City Manuel Pellegrini bado anayo matumaini makubwa ya kumpata mshambuliaji mwingine wa klabu ya Sevilla Alvaro Negredo baada ya kutuma ofa ya paundi milioni 20, kitita ambacho kitaifanya klabu hiyo kutumia paundi milioni 90 katika uhamishio hadi sasa baada ya kuwasajili Jesus Nevas na Fernandinho.
Jovetic close to £25m City switch
MANUEL PELEGRIN
Man City wamemkosa mchezaji Edinson Cavani, ambaye ametimkia klabu tajiri Ufaransa ya Paris Saint-Germain kwa kitita cha paundi milioni 55 lakiniko cha wa Man City Pellegrini anaendelea kutafuta washambuliaji wa kuimarisha safu ya klabu hiyo kuzifumania nyavu baada ya safu hiyo kwa sasa ikiongozwa na Samir Nasri na Edin Dzeko kuonekana kupwaya katika kipindi hiki timu hiyo ikiwa katika maandalizi ya msimu ujao ambapo kwa sasa wameweka kambi huko South Africa.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!