SAMI KHEDIRA-MADRID
Klabu ya Chelsea inatarajia kujichukulia faida kwa Real Madid kumpata Gareth Bale kwa kumnunua Sami Khedira kwa kitita cha paundi milioni 20 ili kuwaongezea fedha ya kumnunulia Bale
Mourinho anataka kuimarisha safu yake ya kiungo kutokana na kiungo wake tegemezi Frank Lampard kuonekana umri kumtupa mkono wakati huo huo Michael
Essien akiwa na majeraha na John Obi Mikel kuwa njiani kuuzwa.
Khedira anaonekana kama chaguo sahihi la Mourinho,mchezaji huyo mjerumani mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Madrid akitokea
Stuttgart mnamo mwaka 2010 na ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa na mahusiano mazuri na Mourinho kwa kipindi chote mreno huyo alipokuwa akiifundisha miamba hiyo ya Hispania
0 comments:
Chapisha Maoni