Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa famili ya mhasibu huyo aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Juma Haji Mkina, Kibibi Juma Mkina, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahani leo Julai 30, 2013 kwa ajili ua kutoka mkono wa pole, kabla ya marehemu kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Rufiji.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika pamoja na waombolezaji nyumbani aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkina, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahati, leo Julai 30 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, baada ya kufika kutoka mkono wa pole na kuwafariji wafiwa kutokana na msiba huo. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji. Picha na OMR
Jumanne, 30 Julai 2013
Related Posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni