Searching...
Jumatano, 17 Julai 2013

KIGOMA WA UKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOANI KATAVI.

 Kiongozi wa shirika la  vijana wajasiliamali Kigoma linalojulikana kama Shirika la Jua kali,  Kapele Shabani (kulia) akitoa maelezo kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu Juma alli Simai (wa pili kulia) kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kuzalishwa na kikundi hicho wakati mwenge wa uhuru ulipozindua rasmi kikundi hicho.
 MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kandaga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Razalo Meshack (kulia) akizungumza katika makabidhiano ya mwenge wa uhuru kati ya mkoa Kigoma na mkoa Katavi katika makazi ya wakimbizi wa Burundi Mishamo wilaya ya Mlele mkoa Katavi (aliyesimama kushoto) ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Alli Simai)
Mkuu wa mkoa Kigoma Issa Machibya (kushoto) akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa mkoa Katavi Rajabu Rutengwe (kulia) baada ya mwenge huo kumaliza mbio za siku nane mkoani Kigoma ambapo ulipitia, kukagua, kuzindua na kufungua miradi 64 yenye thamani ya shilingi bilioni 13.7
PICHA NA DEOGRATIUS NSOKOLO-KIGOMA.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!