Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Mreno Jose Mourinho amejitokeza mstari wa mbele katika mbio za kumtaka mshambuliaji wa Man u Wayne Rooney baada ya kutangaza rasmi kwamba katika dirisha hili la usajili chaguo pekee la Chelsea ni Rooney na sio mchezaji mwingine yoyote lakini akaweka wazi kwamba hawana mpango wa kuongeza dau tena
Kocha huyo wa Chelsea the Blues amesema hawapo tayari kuvunja benk kwaajili ya kumnunua mchezaji huyo na kusisitiza kwamba sasa ni juu ya Man U kunyoa au kusuka.
‘Rooney ni mchezaji mzuri ninayempenda sana lakini siwezi kusema zaidi ya hapoalisema Mourinho.
‘Rooney ni mchezaji mwepesi na mwenye nguvu - ninapenda jinsi ya uchezaji wake,na tunamhitaji Rooney,lakini kwa sasa siwezi kumzungumzia sana kwasababu ni mchezaji wa Manchester United...alimalizia Mourinho
‘Ofa yetu kwa Man U ilikua ya pesa tasilimu na sio kubadilishana na mchezaji wetu,sasa ni juu ya Manchester United; hatutaongeza tena dau.
‘kwa hakika ni ama tumsajili Rooney au tusisajili kabisa’
Mourinho sasa itamlazimu kusubiri kuona kitu gani Manchester United wataamua lakini ni dhahiri kwamba uhusiano wa klabu hizi mbili umevunjika
Chelsea wamekasirishwa zaidi na taarifa zilizozushwa na Manchester United kwamba Chelsea walitaka kubadilishana Rooney na kati ya wachezaji wake Juan Mata au David Luiz taarifa ambazo Chelsea wamekanusha vikali.
Taarifa za uhakika sasa zinasema kutokana na uvumi huo wa kutaka kumchonganisha Mourinho na wachezaji wake Luiz na Matta sasa atahakikisha anamlazimisha Rooney kuondoka Traffod kwa kuzungumza na wakala wake kabla ya mwisho wa wiki hii.
0 comments:
Chapisha Maoni