Searching...
Ijumaa, 19 Julai 2013

JUAN MATA NA DAVID LUIZ HAWAONDOKI CHELSEA-MOURINHO...MAN U WACHOMOA RASMI KUMUUZA ROONEY CHELSEA

Mourinho: Rooney's World Cup 'in trouble' if he stays JOSE MOURINHO-KOCHA WA CHELSEA.
.kocha mkuu wa klabu tajiri ya London ya Chelsea Mreno Jose Mourinho amesisitiza kwamba wachezaji wake Juan Mata na David Luiz ni wachezaji muhimu sana katika mipango yake ya kuijenga timu msimu ujao,na kupuuza taarifa zilizoenezwa na vyombo vya habari kwamba wachezaji hao wapo njiani kuondoka Stamford Bridge.
Luiz ambaye alionyesha kiwango kikubwa sana cha uchezaji akiwa na timu ya taifa ya Brazil katika fainali za kombe la Confederations ambapo waliibuka mabingwa baada ya kuwachapa bila huruma mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Hispania magoli matatu wa sufuri katika mechi ya fainali.United fans' fury at decision to reject Rooney/Mata swap
JUAN MATA.
kufuatia umaridadi mkubwa aliouonyesha katika fainali hizo vilabu mbalimbali vikaonyesha nia ya kumsajili kama vile Barcelona na matajiri wa ufaransa Paris Saint-Germain, wakati Juan Mata yeye wiki iliyopita alivumishiwa kubadilishana na Wayne Rooney huko Manchester United.
Wachezaji wote wawili wapo mapumzikoni baada ya kumaliza fainali hizo za kombe la Confederations na Mourinho amesisitiza kwamba wachezaji hao hawauzwi kwasababu ni wachezaji muhimu sana katika mipango yake msimu ujao.
‘Siwezi kufanya haraka kuwapa mkataba eti kwa sababu tu ya taarifa zinazovumishwa na vyombo vya habari,kwani hata wao wanajua fika kwamba sio za kweli,na nilishawaambia kwamba wao ni wachezaji muhimu sana katika kikosi changu,’ alisema Mourinho.


Rooney isn't worth Chelsea prized assets Mata or Luiz
‘Nilizungumza nao wakati uliopita kipindi cha kiangazi nikiwa likizo na wao wakiwa kwenye kombe la Confederation.
‘walipomaliza mechi yao ya fainali niliwatakia mapumziko mema na kuwaambia tutaonana tarehe 28.07.2013
Mreno huyo tayari alishakanusha taarifa za Mata kubadilishwa na Rooney na kuweka wazi kwamba anamuhitaji mchezaji huyo kuendelea kukipiga na klabu hiyo msimu ujao.
Mata alijiunga na klabu hiyo ya Chelsea mwaka 2011 akitokea klabu ya Valencia kwa mkataba wa miaka mitano
United to refuse to sell Rooney to Chelsea
WAYNE ROONEY.
Klabu ya Manchester United muda mfupi uliopita imetangaza rasmi kwamba wamemuambia mchezaji wao  Wayne Rooney  hawatamuuza kwa Chelsea msimu huu hata kama ataandika barua rasmi ya kuomba kuondoka old tranfod
Tayari Man United wamekataa ofa ya Chelsea kumtaka Rooney japo kilionekana ni kitita kikubwa cha paundi milioni 20.
pamoja na Man united kusisitiza kwamba hawamuuzi Rooney Chelsea,kocha wa Chelsea mreno Jose Mourinho naye ameendelea kukiweka kidonda pilipili baada ya kuendelea kusisitiza kwamba Rooney ndiye chaguo lake namba moja kwa sasa na atahakikisha anatua hapo darajani kwaajili ya kukipiga msimu ujao.
Baada ya Man United kusikia tambo hizo za Chelsea wamemuambia Rooney na wakala wake kwamba Rooney hauzwi kwa gharama yoyote ile na ni lazima abakie klabuni hapo msimu ujao atake asitake kwasababu bado wanao mkataba halali na muingereza huyo
FBL-ASIA-ENG-PR-AUS-MANUTD
DAVID MOYES-KOCHA MAN U.
Katika hali ya kuonyesha bado Moyes ana hasira na Rooney leo hii tena Moyes amesema anaamini kwamba kumjumuisha Rooney kwenye mipango yake msimu ujao ni jambo zuri japokuwa hamtegemei kuwa chaguo lake la kwanza
‘Msimamo wa Klabu juu ya Wayne Rooney haujabadilika,Rooney anao mkataba halali na klabu na sasa amebakusha miaka miwili Old Trafford"alisema Moyes

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!